
"Mimi nina sikio la muziki,Harmonize yuko tofauti,kwanza hajazaliwa na koo la Diamond. Lakini wanamfananisha Harmonize kwa sababu ameishi sana pamoja naye, lazima mtafanana, Hata mimi kuna wasanii nimeishi nao wana pozi kama mimi,pia Harmonize amefikishwa mbali na Diamond kama ataamua kumfuata anavyofanya sio mbaya.Wakati mwingine kuna ukweli kuwa anafanana na Diamond kwa sababu amekua kwa Diamond,sasa mnataka afanane na nameless au?"
Alihoji
Dully Sykes wakati akitambulisha video yake mpya alivyofanya na
Harmomize kwenye kipindi hicho kinachoruka kila ijumaa kuanzia saa tatu
usiku.
0 comments:
Post a Comment