Msanii
wa bongo fleva ambaye anafanya vizuri kuipeperusha bendera ya Tanzania
kimataifa kwenye muziki, ametoa siri ambayo inamfanya awe mstari wa
mbele kumsaidia msanii Chid Benz, alipopata matatizo Diamond Platnumz
amesema anafanya hivyo kwa Chid Benz kutokana na kitendo alichomuonyesha
kabla hajawa maarufu, kukubali kufanya naye collabo ya wimbo wa 'nalia
na mengi', bila kumzungusha na kumtoza hela kama ilivyo kwa wasanii
wengine.
"Mimi nimefanya collabo na Chid, kipindi hicho nilimwambia,
hakunitoza hata sh. kumi wala hakunizungusha hata kidogo, ndio maana
linapokuja suala la Chidi nakuwa wa kwanza, wakati mimi namfuata Chidi,
Chidi hasa nikajua atanikatalia kwanza mimi mbana pua, lakini
hakunizungusha na wala hakuniomba hata mia", alisema Diamond Platnumz.
Tujikumbushe
hivi karibuni msanii Chid Benzi alipata matatizo ya matumizi ya madawa
ya kulevya, na Diamond alichukua jukumu la kumpeleka hospitali na
kumbadilisha damu, kabla hajapelekwa rehab kupata tiba ya urahibu.

0 comments:
Post a Comment