Posted by Williammalecela.com on Friday, August 05, 2016
 |
MAKONDA ATIMIZA AHADI YA KUBORESHA VIWANJA KATIKA NDONDO CUP DAR , CHINA WAKUBALI KUVIBORESHA-
Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo ametiliana saini Mkataba wa
Kuboresha Viwanja Vitatu Ndani YA Jiji la Dar kwa Ufadhili wa Serikali
Ya China, China iliwakilishwa na Balozi wake hapa nchini. Makonda
anastahili pongezi kwa Jitihada zake za Kuhamasisha Michezo kimaendeleo
na Kuamua NDONDO Cup Kusimamiwa na Serikali Ya Mkoa Katika kukuza na
Kuviendeleza Vipaji vya vijana wa Jiji
la Dar,Pia ahadi yake yatimia Ya Kuhakikisha Viwanja vya Michezo Dar
vinakuwa vyenye Ubora baada Ya Serikali Ya China Kuamua Kusaidia kufanya
maboresho baada Ya Rc.Makonda kwenda kuwaomba Kusaidia . Pia kama
Taifa hatuna budi Kumpongeza Makonda kwa kutumia Nafasi aliyonayo siyo
kwa Maslahi yake binafsi bali Kuwa Kiunganishi na Mataifa makubwa
Duniani Maslahi Ya Maendeleo Ya Wana Dar es Salaam. Heko Makonda, Hapa Kazi Tu. |
0 comments:
Post a Comment