Posted by Williammalecela.com on Friday, August 05, 2016
MAKONDA AKUTANA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA (FFU)UKONGA -Awapongeza kwa Uzalendo wao Kwa Taifa letu . -Awaahidi kuwapatia Ambulance
-Awataka Waifanye Dar Kama Dubai Kiulinzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na kikosi cha
kutuliza ghasia(FFU)ukonga Jijini Dar na amezungumza mengi moja kubwa
nao ni Mhe. Makonda amewaeleza kuwa hakuna wafanyakazi wazalendo kama
Askari kwani wao wako tayari kufa ili taifa letu Liwe salama.
Makonda aliongezea kwakusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali
utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu.Rc Makonda
amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba wafanye dar iwe kama
dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta.
Rc.Makonda anaamini dar inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi
bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa
mkubwa. Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga
kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao
huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma
ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais
Dkt.John Magufuli, ombi la Makonda lilikua juu ya asilimia 20% ya
faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji
ikiwa pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili
polisi watakapohitajika wawe wanafika bila kuchelewa.
0 comments:
Post a Comment