Mirror ameliambia Ijumaa kuwa alipata ajali hiyo hivi karibuni akiwa na gari la Wema aina ya Toyota Crown, maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar akitokea Ledger Hotel kufanya mazoezi.

Miraj Juma ‘Mirror’
Mirror
ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Rabininsia Memorial iliyopo Tegeta,
Dar alisema alipata ajali hiyo wakati akimkwepa mama aliyekuwa na
mtoto. Alisema kuwa, baada ya ajali hiyo alipoteza fahamu hadi
alipozinduka na kujikuta hospitalini hapo hivyo akawa akifanya
mawasiliano na Wema kumwelezea hali yake lakini mrembo huyo hakufika
kumjulia hali.Mmoja wa ndugu aliyekuwepo hospitalini hapo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema kuwa, walau Wema angefika kumchangia Mirror fedha za matibabu kwani anadaiwa zaidi ya Sh. milioni 1.3 ili afanyiwe operesheni. Hata hivyo, baadaye Wema aliahidi kufika lakini hakutokea hadi gazeti hili linaondoka hospitalini hapo. Ijumaa lilimtafuta Wema bila mafanikio kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa SMS hakujibu huku watu wake wa karibu wakisema kuwa yupo mikoani kwa ajili ya projekti yake mpya ya kuandaa shoo za vigoma. Jitihada za kumpata bado zinaendelea
0 comments:
Post a Comment