Awanyoshea kidole idara YA ardhi na mabaraza YA Ardhi
- NSSF yatakiwa kuwabana waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakaziMamia YA wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi katika kuwasilisha Kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kufuatia utaratibu aliyojiwekea wa kusikiliza kero siku ya Alhamis ya wiki ya Kwanza na Siku ya Alhamis ya wiki ya mwisho wa mwezi
Katika siku ya leo Kero Nyingi za wananchi ni kuhusu Ardhi ikiwemo utoaji wa hati mbili katika kiwanja kimoja, urasimu wa upatikanaji hati, madai ya fidia na upatikanaji wa hati za kimila
Amwaagiza wakurugenzi na wakuu wa idara za ardhi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wabadilike waongeze kasi ya kushughulikia kero hizo kwa haraka
Pia amewataka kuwa waadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa kwani chanzo cha matatizo mengi yanasababishwa na urasimu, rushwa na kupoteza uzalendo

Katika hatua nyingine ameutaka Mfuko hifadhi ya jamii(NSSF) kuhakikisha wanafuatilia kwa Karibu waajiri wote kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa mujibu wa sheria kwani kila kikao anachokaa kusikiliza kero za wananchi hawakosekani wafanyakazi wenye malalamiko ya waajiri wao kutokupeleka michango ya wafanyakazi wao
Ameishauri mahakama kuharakisha USIKILIZAJI wa kesi na ameagiza jeshi la polisi kuharakisha upelelezi wa kesi



0 comments:
Post a Comment