Malkia
wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Aunt Ezekiel amewamind mashabiki
katika mitandao ya kijamii ambao wanadai anajipendekeza kwa mama watoto
wa Diamond, Zari, baada ya hivi karibuni kuonekana akila nao bata
pamoja.
aunt-na-zari-bongo5
Mwingizaji huyo ambaye alikuwa
rafiki wa Wema Sepetu, amesema lazima awe karibu na familia ya bosi wa
mume wake kwa kuwa hao ndio waliomwajiri mume wake.
“Nataka niwaambie
kitu kimoja maana kujibu mmoja mmoja muda huo sina ni hivi nafanya
nitakalo sifanyi mtakayo, maana nina uhakika nyie mnaokaa kubishana na
mimi vibanda vya mbavu za mbwa vinawashinda, so muda mnaokaa mkafatilia
yangu mngeenda kutafuta yakufanya, ooh! njaa yes i say tena yes maana
mnataka nibadili red kuwa yellow kwani yule si ni boss wa mkata viuno
wangu au!. Sasa kama ni bosi ulitaka nibishe niseme mimi ndio bosi, basi
nifungue bendi yetu acheze!,” Aunt Ezekiel aliandika instagram.
Aliongeza,
“Mnawazimu nini na namweshimu kama mshkaji rafiki bosi wa bwana yangu
na siwezi acha kushirikiana na familia yake eti kisa ushuzi mtasema
nini. Sitaki kutaja majina ya watu ila kilichopo ndio ukweli asilia,
Mama Tee ndio mwanamke na mama watoto wa Nasibu no way hata tulambe lami
kubadili ni ngumu ila mwenyewe akibadili basi na sisi tutabadili ila
kwa sasa ni Mama tee shukrani gud Day,”.
Mwigizaji huyo anatoka
kimapenzi na densa wa Diamond, Mose Iyobo ambapo mpaka sasa wamefanikiwa
kupata mtoto mmoja aitwae Cookie.
0 comments:
Post a Comment