Najua
ngoma ya Diamond ya “Salome” ni kali zaidi na imesababisha Tanzania
kumkumbuka tena Legendary Saida Kalori kwani kwa wakati ukizisikia Maria
Salome na Salome ya Diamond zikipigwa kwa pamoja au moja moja ni
kawaida kwani hii ni win win Situation kwa wasanii wote wawili, Sasa
Diamond amefunguka kwamba kuna shavu jingine jipya linakuja kati yake
yeye na Legendary Saida Kalori.
Akiongea na Perfect255, Diamond
Platnumz amesema kwamba anafikiria siku ambayo atakuja kuperforme Dar
jukwaani basi lazima atamuhusisha na Legendary Saida Kalori na kingine
Kikubwa Diamond platnumz amesema kwamba inawezekana pia yeye na Saida
Kalori kufanya kolabo ya pamoja.
“Tulizungumza hilo pia na ninafikiri
siku ya kwanza nitakayo performe nyimbo Dar es salaam inawezekana
nikamleta Saida tukaperforme pamoja” Alisema Diamond
0 comments:
Post a Comment