Msanii
Dully Sykes ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Inde’
amefunguka na kusema kuwa yeye atakufa kwenye muziki kwani hawezi kuacha
kufanya muziki kwa kuwa muziki ndiyo maisha yake.
Akiongea kwenye
Planet Bongo Dully Sykes amesema kuwa yeye hakusoma shule hivyo hawezi
kusema anaacha muziki au kustaafu muziki bali yeye atakomaa na muziki
mpaka siku yake ya mwisho katika dunia hii.
“Mimi siyo kama Fid Q yule amesoma hivyo
anaweza kusema aache muziki akafanya kitu
kingine
alichosomea sasa mimi shule sikwenda mimi nitafanya muziki kwani maisha
yangu mimi ni muziki, muziki ni kazi yangu, naendesha maisha yangu na
familia yangu kwa sababu ya muziki, na kama ningetaka kufanya kitu
kingine
nadhani ningekuwa nimeshakata tamaa na muziki lakini mimi na
muziki ni kama nimesomea darasani, baba yangu mwenyewe amekufa anafanya
muziki na mimi nitakufa nafanya muziki siwezi kuacha” alisema Dully
Skyes.
Mbali na hilo Dully Skyes amesema kuwa kwa sasa hafikiri kutoa
albam kwani haamini kama inaweza kuwa biashara labda mpaka aone kuna
msanii ametoa albam na amefaidika na mauzo ndiyo yeye anaweza kuja kutoa
albam.
“Mimi sitaki kujaribu suala la albam kwani kwa upande wangu
sioni kama ni biashara kwa sasa ila wakati mimi naanza muziki uongo
albam ilikuwa biashara kweli, nikitoa leo albam nikija kutambulisha tu
hapa nikitoka nje hapo tayari itakuwa imeshazagaa.
Kipindi chetu albam zilikuwa zinalipa sana na tumefaidika sana ila akitokea saizi mtu akatoa albam na akasema
imemlipa hapo ndiyo nitawaza ila mimi siwezi kujaribu kutoa albam saizi” alisema Dully Skyes.
0 comments:
Post a Comment