Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Matatizo’.Amefunguka na kusema kuwa katika harakati zake za kutafuta maisha alishawahi kuwa dereva wa bodaboda.
Harmonize amesema aliifanya kazi hiyo katika kuhakikisha anaendesha maisha yake kabla ya yeye kutoboa kwenye mambo ya muziki.
Akiongea
kupitia kipindi cha ‘Ngazi wa Ngazi’ Harmonize alisema kuwa anakumbuka
mwaka 2011 alikuwa akifanya kazi hiyo ya kuendesha pikipiki na kubeba
abiria ndiyomaana ana uzoefu mzuri wa
kuendesha Pikipiki kutokana na
kazi yake hiyo aliyoifanya kwa muda fulani.
“Unajua mimi nilishawahi
kuwa dereva bodaboda nakumbuka ilikuwa mwaka 2011 nilikuwa nafanya kazi
ya kubeba watu na Pikipiki hivyo nina uzoefu mzuri tu wa kuendesha
Pikipiki, nilikuwa nabeba abiria hapa na pale najipatia riziki ndiyo
maana hata katika video yangu ya ‘Bado’ niliona niendesha tu ile
pikipiki kwa kuwa nilikuwa na uzoefu wa kuendesha pikipiki, ” alisema
Harmonize.
0 comments:
Post a Comment