“Nimeamua
kuweka mambo hadharani kwa sababu kila kukicha Meneja wa Tip Top, Babu
Tale ananisema kuwa nimemrudisha Chid kwenye matumizi ya madawa ya
kulevya kitu ambacho sio sahihi, mimi kwake nafuata mapenzi tu sasa
nikisikia anaenda kwa Uwoya naumia maana mzigo nitakuwa nabebeshwa mimi
kumbe pengine anayetakiwa kulaumiwa ni Uwoya,” alisema Bhoke. Akizidi
kushusha ubuyu huo wa motomoto, Bhoke alisema kilichomfanya ashtukie
mchongo, kuna siku alikuwa na msanii huyo kwenye gari, ghafl a Uwoya
alimpigia simu Chid wakawa wanazungumza na kumuuliza kuwa atakwenda
nyumbani kwake saa ngapi kitu ambacho kilimkera sana.
“Jamani
mtu niko naye njiani tumetoka kwenye raha zetu, ghafl a naona simu ya
Chid inaita, kuangalia ni Uwoya na nilipomuuliza aliniambia ni mtu
ambaye anamsaidiaga sana kumpa fedha na wakati mwingine huwa anaenda
kwake kukaa siku mbili mpaka tatu. “Kama mwanamke nilishindwa
kumvumilia, tuligombana sana na Chid, aliniboa na huyo Uwoya nikamchukia
pia. Nimemwambia Chid achague upande kati ya mimi au Uwoya, mimi
namsikilizia,” alikuja juu Bhoke.
Amani
lilimtafuta Uwoya kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya Bhoke ambapo
alipopatikana aling’aka kwa kusema anashangaa madai hayo kwani hata kwa
hivi sasa hajui Chid yuko wapi na pia hadhani kama anapafahamu anapoishi
na kamwe hawezi kutoa fedha yake hata siku moja kumpa Chid japokuwa
walishawahi kuwa marafi ki sana huko nyuma.
“Chid
sidhani hata kama anapafahamu kwangu japokuwa alikuwa rafi ki yangu sana
kitambo huko na pia mimi siwezi kutoa fedha kumpa Chid kwa sasa, hivyo
itakuwa wanadanganyana yeye na mpenzi wake maana hata sasa hivi sijui
huyo mtu alipo,” alisema Uwoya. Alipotafutwa Chid ili kujua
anazungumziaje madai hayo ya Bhoke, simu yake haikuwa hewani. Jitihada
zinaendelea ili kumsikia kwa upande wake.
0 comments:
Post a Comment