Malkia
wa mipasho nchini, Khadija Omar Kopa amefunguka kuhusiana na sababu ya
kushuka kwa muziki wa taarab na kuongelea michakato yake ya kuupeleka
muziki huo kimataifa.
Akipiga story na eNEWZ, Khadija Kopa amesema
kuwa muziki wa taarab hauwezi kufika kimataifa pasipo kuwepo na mchango
wa wadhamini wakaufanya ufike kimataifa.
“Tunamuomba Mungu na tunaomba wafadhili
kama
wapo wajitokeze kwenye taarab maanataarab inalipa, Hauwezi kufika
kimataifa bila kuwa na wadhamini” Alisema Khadija Kopa.Ikumbukwe kuwa
miezi ya nyuma mwanamuziki
Diamond Platnumz alishafanya wimbo na
Khadija Kopa wimbo walio upa jina la ‘Nasema Nawe’ nakufanya vizuri
katika kiwanda cha muziki nchini.
0 comments:
Post a Comment