
Baada
ya kuripotiwa na gazeti hili kuwa ni mjamzito, staa wa kitambo wa
sinema za Kibongo, Yvonne Cheryl ‘Monalisa’, sasa ameamua kukionesha
kitumbo chake huku mashabiki wakidai kuwa anashindana na Zarinah Hassan
‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni kawaida yake kuonesha tumbo lake.
Juzikati Mona alijipiga picha akatupia mtandaoni akidai kuwa ameshiba
matunda, hivyo kuibua maneno mengi kwa mashabiki wake waliotaka kujua
baba wa mtoto huyo. Kwa mujibu wa wafanyakazi wenzake, Mona ana furaha
ya kupata ujauzito huo. Wikienda linamtakia heri katika safari yake ya
kuelekea kwenye malezi ya mtoto wa tatu
0 comments:
Post a Comment