Posted by Williammalecela.com on Wednesday, September 07, 2016
Kiongozi wa Ufilipino Rodrigo
Duterte amesema anajutia kwamba amatamshi yake kumhusu kiongozi wa
Marekani Barack Obama yamefasiriwa kama matusi.
Bw Duterte amesema
hayo baada ya Bw Obama kufuta mkutano wake na kiongozi huyo kutokana na
maneno ya lugha chafu yaliyoelekezwa kwake. Kiongozi huyo wa
Ufilipino alikuwa amemweleza Bw Obama kama "mwana wa kahaba" na kuongeza
kwamba hatakubali kuulizwa maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za
kibinadamu nchini mwake. Alisema Ufilipino haitawaliwi na mtu yeyote. Ufilipino ilikuwa koloni ya Marekani.
Hayo yalijiri kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa bara Asia, mjini Laos. Lakini kupitia taarifa, Bw Duterte amesema anajutia matamshi hayo. Amesema wanadiplomasia wa Ufilipino na Marekani wanatarajia kuondoa uhasama na tofauti zilizozuka baina ya nchi hizo mbili. Rais Barack Obama alionywa na Bw Duterte "kuonyesha heshima"
Tangu kuingia madarakani, Bw Duterte ameendelea
kutumia maneno makali, na kutumia lugha chafu kuwarejelea Papa Francis,
maafisa kadha wa Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
John Kerry na balozi wa Marekani nchini Ufilipino.
Rais wa Marekani Barack Obama
amevunja mkutano wake na Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, ambaye awali
alikuwa amemwita "mwana wa kahaba".
Bw Obama awali alikuwa
amesema kwamba angemuuliza kiongozi huyo maswali kuhusiana na mauaji ya
kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa dawa za
kulevya Ufilipino. Lakini Bw Duterte, ambaye ameunga mkono mauaji
hayo, alisema iwapo hilo lingefanyika: "Putang ina (mwana wa kahaba)
nitakutusi katika mkutano huo." Maafisa wa Obama wamesema badala yake kiongozi huyo sasa atakutana na rais wa Korea Kusini. Msemaji
wa baraza la taifa la usalama Marekani Ned Price ameambia wanahabari
kwamba Bw Obama atakutana na Bi Park Geun-hye katika mkutano wa Mataifa
ya Kusini Mashariki mwa bara Asia (Asean) mjini Laos, ambapo viongozi
wamekusanyika kwa mkutano mkuu.
Bw Obama, aliyetua Laos baada ya
kuhudhuria mkutano wa G20 mjini Hangzhou, China, alitarajiwa kuuliza
maswali kuhusu
ukiukwaji wa haki za kibinadamu Ufilipino. Lakini akiongea mjini Manila Jumatatu kabla ya kuondoka kuelekea
Laos, Bw Duterte alishutumu hilo na kusema ni "kukosa adabu" na
akamtusi rais huyo wa Marekani. Aliongeza kwamba: "Tutagaragazana
matopeni kama nguruwe iwapo utafanya hilo." Kisha, alizungumzia
kampeni ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya ambapo washukiwa
2,400, wakijumuisha walanguzi na watumizi, wameuawa nchini Ufilipino
tangu achukue mamlaka mwezi Juni.
"Kampeni dhidi ya dawa za
kulevya itaendelea. Wengi watafariki, wengi watauawa hadi tuangamize
mlanguzi wa mwisho na kumuondoa kutoka barabarani ... hadi mtengenezaji
wa mwisho wa dawa hizi auawe, tutaendelea."
Bw Obama awali
alidunisha matusi hayo na kusema aliwaomba maafisa wake kuchunguza iwapo
huu ni wakati mwafaka wa kuwa na mashauriano ya kufana. Baadaye, maafisa wake walivunjilia mbali mkutano huo. Ziara
ya mwisho ya Obama bara Asia akiwa kama rais imejaa vioja. Alipowasili
Uchina, alijipata kwenye mzozo wa itifaki kati ya maafisa wa Marekani na
Uchina ambapo alikosa kuwekewa zulia jekundu.
Matusi
Hii si mara ya kwanza kwa Rais Duterte kutumia lugha chafu kuwarejelea viongozi mashuhuri. Alimwita
Papa Francis "mwana wa kahaba", waziri wa mambo ya nje wa Marekani John
Kerry "mwendawazimu" na majuzi alimweleza balozi wa Marekani nchini
Ufilipino kama "mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa kahaba".
Image copyrightAPImage caption
Wachanganuzi wanasema tabia ya Duterte inamfanya
kupendwa sana nyumbani lakini huenda akatengwa na jamii ya kimataifa
Wachanganuzi wanasema tabia ya Duterte inamfanya kupendwa sana nyumbani lakini huenda akatengwa na jamii ya kimataifa. Umoja wa Mataifa tayari umeshutumu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini humo.
Mwezi
Agosti, wataalamu wawili wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa
walisema agizo la Bw Duterte kwa polisi na umma kuwaua washukiwa wa
ulanguzi wa dawa za kulevya ni "uchochezi wa ghasia na mauaji, na ni
uhalifu chini ya sheria za kimataifa."
0 comments:
Post a Comment