Huwa
wanayatamka maneno hayo ili waweze kuuvaa uhusika wa kifi lamu. Yaani
kama anatakiwa kuonekana analia, msanii ajitoe ufahamu kwa muda ili
aonekane analia mbele ya kamera. Mathalani, anaweza kuvaa uhusika wa
tabia za mlinzi wakati yeye si mlinzi.
Kwa
tafsiri rahisi ni kwamba anachokifanya pindi anapoambiwa maneno hayo
huwa si uhalisia. Anakuwa anaigiza. Anavaa uhusika wa jambo fulani
baadaye anarudi kwenye hali yake ya kawaida. Huo ndiyo msingi wa mimi
leo kumuandikia barua nzito muigizaji mwenye umbo la kuvutia,
aliyejaajaa mwili, mwenye rangi ya ‘chokoleti’, mtoto wa mzee Ford, wa
kuitwa Shamsa.
Awali,
nianze kwa kukupongeza. Umefanya uamuzi wa busara sana kuingia kwenye
chama cha wenye ndoa, umemkabidhi moyo wako kijana mtanashati na
mchakarikaji wa mjini, Chid Mapenzi. Najua hadi kufi kia hatua hiyo,
unayo mapito mengi, lakini mwisho wa siku, nyinyi sasa ni mke na mume.
Kama nitakuwa sahihi, hamkuchukua muda mrefu sana kwenye uchumba.
Kama nitakuwa sahihi, hamkuchukua muda mrefu sana kwenye uchumba.
Sina
hakika kama mmefi kisha hata miezi sita lakini hilo haliondoi dhana
nzima ya muunganiko wenu. Mlikaa, mkatafari na mwisho mkaona hakuna
sababu ya kuendelea kuwafaidisha wamiliki wa nyumba za wageni. Mkachagua
kuishi pamoja, mpike na kupakua bila kuulizwa na mtu. Hongereni sana!
Baada ya pongezi hizo, acha nihamie upande wa pili wa barua yangu; ‘ndoa
na ustaa’.
Nimeona
nikutahadharishe mapema. Ni vitu viwili tofauti. Chondechonde
usithubutu kuchanganya vitu hivi. Ni hatari. Dada yangu, unapokuwa
nyumbani kwa mumeo yale mambo ya utani wa lokesheni achana nayo kabisa.
Zile za kuitana ‘baby’ mnapokuwa lokesheni, hupaswi kuzifanya
unapokuwa na mumeo nyumbani.
unapokuwa na mumeo nyumbani.
Achana
na mambo ya kufuga kucha ndefu halafu eti ukawa mtu wa kupikiwa kila
siku na hausigeli. Ikiwezekana chakula cha mumeo mpikie mwenyewe.
Kupikiwa na mkeo nako kuna raha yake. Kunaongeza upendo pia, hata kama
unatingwa na kazi zako lakini tenga siku za wewe kuingia mwenyewe jikoni
na kumkorofi shia shemeji yetu. Usitumie mwanya wa kazi zako kufanya
mambo ambayo hayatamfurahisha mwenzio.
Jiheshimu.
Uigizaji uwe na mipaka. Siyo unaruhusu waigizaji wenzako wakutanie
kiasi cha kuondoa thamani ya kuwa mke wa mtu. Weka mipaka ya kazi na
ndoa. Mashosti
zako wasiwe madereva wa ndoa yenu. Wasijigeuze rimoti na kuanza kuwachezesha wanavyotaka. Usiruhusu ule ushauri wao wa mtu kutaka muishi kama anavyoishi yeye. Ishini nyinyi kama nyinyi. Kila mmoja wenu ameacha familia yake, mmekwenda kuanzisha familia mpya. Nyinyi ndiyo muwe madereva wa ndoa yenu. Muamue mnataka kuishi vipi. Hiyo ni taasisi yenu mmeianzisha, nyinyi ndiyo wakurugenzi. Hakuna mtu juu yenu atakayewapa amri ya kuishi.
zako wasiwe madereva wa ndoa yenu. Wasijigeuze rimoti na kuanza kuwachezesha wanavyotaka. Usiruhusu ule ushauri wao wa mtu kutaka muishi kama anavyoishi yeye. Ishini nyinyi kama nyinyi. Kila mmoja wenu ameacha familia yake, mmekwenda kuanzisha familia mpya. Nyinyi ndiyo muwe madereva wa ndoa yenu. Muamue mnataka kuishi vipi. Hiyo ni taasisi yenu mmeianzisha, nyinyi ndiyo wakurugenzi. Hakuna mtu juu yenu atakayewapa amri ya kuishi.
Nyinyi
ndiyo mnapaswa kujitolea amri. Kabla sijamaliza barua yangu, nikupe
jambo lingine la msingi sana katika maisha yako. Mtangulize Mungu mbele
katika kila jambo. Yeye ndiye jibu la majaribu yote mtakayokutana nayo.
Hakuna
litakalowashinda endapo mtamkabidhi maisha yenu Mungu wetu wa mbinguni.
Mkiwa na shida, muombeni yeye atawapa suluhu. Atafanya njia pasipokuwa
na njia. Yeye ndiye njia ya kweli na uzima. Nikutakieni kila la kheri
katika ukurasa mpya wa maisha mlioufungua, Mungu awabariki! Mimi ni
kaka’ko;
Barua nzito na ERICK EVARIST Maoni&Ushauri: 0768 811595
0 comments:
Post a Comment