Born: January 26, 1963 (age 53), Setúbal, Portugal
Height: 5′ 9″
Full name: José Mário dos Santos Mourinho Félix
Spouse: Matilde Faria (m. 1989)
Teams coached: Manchester United F.C. (Manager, since 2016),
Posted Jumanne,Septemba27 2016 saa 12:31 PM
Kwa ufupi;-
Kila mtu anatetea kibarua chake, hivyo Mreno huyo amegundua kwamba kuendelea kukumbatia matatizo yatamgharimu zaidi katika kazi yake ya kuinoa Manchester United, hivyo amekunjua makucha kwa kuwapiga chini mastaa wote anaodhani ni shida na anafanya hivyo bila ya kutazama sura ya mtu.
J
OSE
Mourinho hataki ujinga kabisa kwenye kazi yake. Kibarua chake
kimetikisika na kuona hivyo akatazama nani ni tatizo, akaibuka na uamuzi
mmoja wa kumpiga chini nahodha wake Wayne Rooney.
Kila
mtu anatetea kibarua chake, hivyo Mreno huyo amegundua kwamba kuendelea
kukumbatia matatizo yatamgharimu zaidi katika kazi yake ya kuinoa
Manchester United, hivyo amekunjua makucha kwa kuwapiga chini mastaa
wote anaodhani ni shida na anafanya hivyo bila ya kutazama sura ya mtu.
Kwanza
ameanza na nguli wa klabu hiyo, Rooney na panga litampitia pia kiungo
Mbelgiji Marouane Fellaini, watasubiri sana benchi. Mourinho amempiga
marufuku Rooney kuzungumzia viwango vya wenzake wakati yeye mwenyewe
yupo hovyo zaidi, huku Fellaini ambaye alikuwa na zali la kuanzishwa
mechi zote za mwanzoni akicheza sambamba na Paul Pogba kwenye kiungo,
zamu ya kusugua benchi imemfikia rasmi baada ya kocha huyo kudai kwamba,
ameona Pogba anaelewana zaidi na Ander Herrera.
“Pogba
kucheza vizuri? Hakucheza vibaya dhidi ya Southampton. Hakucheza vibaya
pia dhidi ya Hull City. Ipo hivi, timu inapocheza vizuri, naye anakuwa
mzuri zaidi. Tunatarajia mengi kutoka kwake, lakini nimeona Pogba na
Herrera wanaelewana zaidi, pacha wa uwanjani.”
Kuhusu
Rooney, Mourinho anaripotiwa kuketi kitako na staa huyo na kisha
kumweleza kwamba, kitu ambacho anatakiwa kufanya kwa sasa ni kuhangaika
kupandisha ubora wa kiwango chake na si kuendelea kuwahubiria wachezaji
wenzake kucheza vizuri wakati tatizo kubwa linaanzia kwake. Rooney
anaripotiwa kutumia muda mwingi vyumbani kuwasema wenzake kuhusu viwango
vyao wakati timu hiyo ilipochapwa 2-1 na Manchester City, wakati
mwenyewe alikuwa hovyo kwenye mechi hiyo na mechi nyingine zilizofuatia
kabla ya kupiga benchi dhidi ya Leicester City Jumamosi iliyopita.
Ripoti
zimefichua kwamba Rooney mwenyewe amekubaliana na ukweli kuhusu kiwango
chake na anatambua itakuwa ngumu kupata nafasi katika kikosi cha
kwanza, lakini hawezi kufikiria kuondoka kwenye timu hiyo hadi mkataba
wake utakapofika tamati ambapo kwa sasa umebakiza miaka miwili.
Gwiji
la Man United, Gary Neville, ambaye aliwahi kucheza na Rooney kwenye
klabu hiyo na kwenye timu ya taifa ya England kabla ya kuwa kocha,
alisema fowadi huyo itabidi akubaliane tu na hali halisi ya kuchezeshwa
kwa awamu na Mourinho.
“Hiki
ni kipindi cha mpito katika maisha yake ya soka, kipindi ambacho umuhimu
wake utakuwa katika mtazamo tofauti,” alisema Neville.
Wakati
Rooney na Fellaini ikionekana kubana upande wao, kuna wachezaji wanne
wanaonekana kuwa na nafasi kubwa na kupewa nafasi zaidi katika kikosi
cha kwanza ambao ni Juan Mata, Marcus Rashford, Jesse Lingard na Zlatan
Ibrahimovic. Hizi sura zitaonekana sana kwenye timu ya Mourinho.
Imefichuka kwamba Rooney atarudi kikosi kwenye mechi ya Europa League
dhidi ya Zorya Luhansk, lakini atarudi benchi kwenye Ligi Kuu England
dhidi ya Stoke City Jumapili.

0 comments:
Post a Comment