Posted by Williammalecela.com on Tuesday, September 27, 2016
 |
| ;Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana
katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika
ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China
wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika
Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka
kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa. |
 |
| Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura
akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti,
Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya
StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya
Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016. Washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao
watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China
wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa
Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili, &;Meneja Mkuu wa
Shirika la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa
Ubalozi wa China nchini, Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa
Makampuni ya StarTimes, Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni
katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya
Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing
2016 |

 |
| Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ;Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao. |
0 comments:
Post a Comment