Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea kwani una changamoto nyingi
hasa pale unapofikia wakati wa kumtafuta mtu sahihi wa kuwa naye
maishani yaani mke au mume.
Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper anaweza kuthibitisha
hilo kwani pengine anaweza kuwa staa mwenye listi ndefu ya wanaume
waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata walichokitaka na mitini japo
haikatishi ndoto zake za kumpata mtu sahihi wa kuwa nae kwenye
mahusiano.
ABDALLAH MTORO ‘DALLAS’
Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na fedha ‘chafu’ na alianzisha uhusiano na
Wolper ambapo alimvisha pete ya uchumba na kumtambulisha mpaka kwa
wazazi wake naye kujitambulisha kwa wazazi wa mwanadada huyo lakini
walimwagana baada ya Wolper kuhisi kwamba anasalitiwa kwa mpenzi wake
huyo kuwa na uhusiano na wasanii wenzake.
GEE MODO
Jamaa huyo ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya viatu na nguo maeneo
ya Kinondoni jijini Dar ambapo baada ya Wolper kuachana na Dallas naye
aliingia kwa gia ya kumvisha pete ya uchumba na mapenzi kuwa motomoto
kwa kile kilichoonekana kwamba anampooza machungu.
Hawakukaa muda mrefu, wawili hao waliachana japokuwa sababu za
kumwagana kwao hazikujulikana ila tayari jamaa huyo alikuwa ameshamfaidi
penzi la mrembo huyu.
JIMMY MGAYA
Jimmy ni Mbongo aishiye Afrika Kusini ‘Sauz’ ambaye naye ni
mfanyabiashara pia,Baada ya Wolper kuachana na Gee Modo alinasa kwa
Jimmy ambapo kwa mara ya kwanza zilinaswa picha zao za kimahaba wakiwa
nchini Afrika Kusini.
MWAMI RAJABU
Mwami ni mfanyabiashara wa madini ambaye ni raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo. Mara nyingi Mwami alionekana jijini Dar es
salaam kwa kazi zake za kibiashara ambapo hufikia hoteli za kifahari
ambapo Mwami anatajwa kwamba aliwahi kumvisha pete ya uchumba Wolper
lakini hakuna kilichoendelea baada ya jamaa huyo kudaiwa kupata
alichokitaka.
MKONGO
Katika kujaribu tena bahati yake, Wolper alijikuta mapenzini na Mkongo
mmoja ambaye mpaka wanaachana jina lake halisi halikupatikana ambapo
kama ilivyokuwa kwa wengine waliotangulia,mahusiano yao haukuchukua muda
mrefu na walitengana.
Mkongo
huyo alimvisha Wolper pete ya uchumba na alikuwa akisema mara kwa mara
kuwa wapo kwenye mipango ya ndoa hata pale ukweli ulipogundulika kwamba
ni mume wa mtu ambapo Wolper alidai hatasikiliza maneno ya watu,ila
mwisho wa siku wakaja kumwagana baada ya Mkongo kumfaidi mrembo huyo.
MY TAKE :
Jackine Wolper kama muigizaji nnaeamini ana kipaji cha hali ya juu,ni
wazi kuwa endapo akiwa kwenye mahusiano na mtu sahihi hata shughuli
zake za kisanaa anaweza kuzifanya kwa ufanisi na kukata kiu ya mashabiki
wake ambao wamechoshwa na drama za mgazetini na kwenye mitandao ya
kijamii,hivyo kama kweli anaamini Harmonize ni mtu sahihi kwake huu ni
muda muafaka wa kukaa chini na kutulia nae kwani licha ya wote wawili
kuwa mastaa,ni wazi kuwa mahusiano yao yatakua na manufaa ya kibiashara
kwenye kazi zao za kisanaa.

0 comments:
Post a Comment