Madai
mazito! Kufuatia baadhi ya mastaa wa kike Bongo kuwa na tabia kila
anapokuja staa wa nje kwa ajili ya kupafomu au mwanaume mwenye fedha
kufanya jitihada za kumnasa kimapenzi, wanadaiwa kuwa ni ‘jamvi la
wageni’ kwa kile kinachosemekana kuwa huwa wanajilengesha wenyewe,
Wikienda lina listi kamili.
Chanzo makini kimelidokeza Wikienda kuwa
baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakijilegeza kutoa penzi kwa mastaa
wanaotoka nje ya nchi kwa sababu tofauti. Wengine wanaamini ni kupata
umaarufu. Wengine kupata mkwanja mrefu kuliko wanaume wa hapa nyumbani
na kuna wanaotaka ‘koneksheni’ za nje ya nchi. “Kiukweli Gazeti la
Wikienda tunajua ninyi huwa hamuogopi kusema. Yaani hawa mastaa wa kike
wamekuwa ni jamvi la wageni maana kila staa wa nje anayekuja Bongo
lazima utasikia amelala na huyu mara yule, jambo ambalo linatupotezea
sifa kwani tunaonekana ni washamba wanaopenda kushobokea mapenzi,”
kilisema chanzo hicho na kuanika listi kamili. Bila kupepesa, chanzo
hicho kilisema kuwa kuna mastaa kibao waliowahi kutajwa kwenye skendo ya
kulala na staa wa nje aliyetua nchini au wanaume mapedeshee wanaotua
nchini.
LISTI KAMILI “Nawasaidia listi. Yumo Gigy Money (video
queen wa Bongo, Gift Stanford) ambaye alidaiwa kulala hotelini na
Mwanamuziki wa Nigeria, Tekno Miles. “Listi nyingine ni Linah na Wizkid
(alipotua mwaka jana), Shilole na Wizkid (mwaka huu), Masogange na yule
mwanaume raia wa Uganda, Wema na Mshiriki wa BBA, raia wa Nigeria, Luis
Mnana, Amber Lulu na Run Town na wengine wengi kama akina Wolper, Jini
Kabula, Mary Mawigi, Kidoa na Lulu Diva,” kilidai chanzo hicho. Baada ya
kumwagiwa ubuyu huo mzito, Wikienda lilizungumza na baadhi ya mastaa
hao kuhusiana na suala hilo ambapo kila mmoja alikuwa na lake la
kuzungumza. Gigy Money: “Siyo kwamba tunawashobokea hao wanaume bali
mastaa wa nje ndiyo wanaotushobokea wenyewe kwa sababu mademu wa Bongo
ni wazuri. Nilipolala na Tekno walinitafuta wao wenyewe. Kitu kingine
hawa Wanigeria wanajua kujali sana wanawake. Pia wanaume wa kutoka nje
ya Bongo wanatoa fedha nzuri na ya maana siyo kama Wabongo.” Amber Lulu:
“Wanaume mastaa wa nje wanajali sana wanawake kwa kweli na wanatoa
fedha nzuri siyo kama wanaume wa Bongo ambao hawako romantic ndiyo maana
tunawashobokea. Nimewahi kuwa kimapenzi na staa anayejulikana kwa jina
la Run Town, nili-enjoy mno.” Mary Mawigi: “Mapenzi ni popote, unaweza
ukampenda yeyote hiyo ni hali ya kawaida tu haijalishi yukoje.”
0 comments:
Post a Comment