![]() |
BONDIA Francis Cheka amemuomba Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kuwakomboa wanandundi kutoka mikononi
mwa mapromota wababaishaji.
Cheka ametupia ujumbe huo kwenye mtandao wa
kijamii wa Facebook, akimuomba Nape awakomboe kwa kuwa kumekuwa na mapromota
ambao hushikilia pasi zao za kusafiria huku wakijua si sahihi.
"Waziri wangu, embu angalia mapromota
wanavyo tutesa, wanakaa na Viza na Passport zetu, ambayo ni haki zetu kama
raia," ameandika Cheka.
Cheka amevunja ukimya huo na kuweka wazi tabia
za mapromota wa mchezo huo ambao wamekuwa kikwaza cha mchezo huo.
"Tunakosa mapambo ya nje, Waziri wa
Michezo tukomboe ili tukuletee mikanda mingi, pesa za kigeni, heshima na
tuitangaze zaidi nchi yetu huko nje."

0 comments:
Post a Comment