MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda amekagua vituo vidogo vya polisi katika mkoa huo na kubaini kuwa
havikidhi haja ya kuwahudumia wananchi na kuahidi kujenga vituo vipya 20.
Amesema kuwa vituo hivyo vitakuwa na thamani ya shilingi bilioni 10 kwa wastani wa shilingi milioni 500
kila kituo kimoja vitakavyokuwa na askari 100 kwa kila kituo na silaha za
kutosha.
Amesema kuwa kufanya hivyo
kutasaidi kuzuia mianya ya wahalifu wanaovamia vamia vituo hivyo na kwamba
ameeleza kuwa vituo hivyo vitafanya kazi usiku na mchana katika mazinguira
mazuri.
“Tayari ninampango wa
kujenga vituo ishirini vikubwa katika mkoa wa Dar es Salaama ambayo vitakuwa
vikifaanya kazi usiku na mchana vitakavyokuwa na askari wasio pungua 100 na
watafanya kazi usiku na mchana katika mazingira mazuri”amesema Makonda.
0 comments:
Post a Comment