| JENGO LA MAHAKAMA YA KISUTU |
MBELE ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
mfanyabiashara mashughuli Ndama Hussein
anayetafahamika kwa jina la Ndama Mtoto wa Ngombe amepandishwa kizimbani
akikabiriwa na mashtaka sita.
Mfanyabaishara Ndama Hussein maarufu kama
mtoto wa Ng’ombe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar
es Salaam, akikabiliwa na mashtaka sita ikiwamo kughushi na kutakatisha Dola za
Kimarekani 540,390 (sawa na Sh, bilioni 1.181).
Wakili wa serikali Christopher Msigwa
akimsomea mashataka mtuhumiwa hiyo mbele
ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria
Nongwa ambapo Msigwa alidai kuwa Februari 20, mwaka 2014, jijini Dar es Salaam,
mshtakiwa akiwa na lengo la kudanganya alighushi nyaraka za kusafirisha madini
akionyesha kwamba Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited imepewa
kibali cha kusafirisha boksi nne za vipande wa dhahabu zenye uzito wa kilo 207
zenye thamani ya Dola za Kimarekani 8.2 kwa Kampuni yenye makazi yake nchini
Austaria inajulikana kama Trade TJL DTYL Limited huku akijua nyaraka hizo za
uongo.
Shtaka la pili, alidaiwa kufanya Machi 6,
mwaka 2014, jijini Dar es Salaam akiwa na nia ya kudanganya, aliandaa nyaraka
za uongo kuonyesha kwamba hati ya kuondolea mizigo kutoka ofisi za Umoja wa
Mataifa za tarehe hiyo, akiwa na lengo la kuonyesha kwamba vipande vya dhahabu
vyenye uzito wa kilo 207 kutoka Jamhuri ya Congo, kuwa zinasafirishwa na
Kampuni ya Muru Platnum kwenda Austraria.
Msigwa alidai katika shtaka la tatu, Februari
20, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kudanganya alighushi
nyaraka zikionyesha kuwa ni fomu ya tamko la kodi akionyesha Kampuni ya Muru
Platnum imelipa Dola za Kimarekani 331,200 kama kodi ya kuingiza mzigo kwa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kilo 207 ya vipande vya dhahabu vyenye
thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
huku akijua ni uongo.
Katika shtaka nne, Februari 20, mwaka 2014
jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka
zauongo za kuonyesha kuwa ni za bima kutoka Kampuni ya Phoenix Ltd za
terehe hiyo, akilenga kuonyesha kwamba Kampuni ya Muru Platnum imekatia bima
boksi nne za vipande vya dhahabu zenye uzito wa kilo 207 vyenye thamani ya Dola
za Kimarekani 8,280,000 huku akijua ni uongo.
Katika shtaka la tano na sita, kati ya
Februari 26 na Machi 3, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, alijipatia kwa njia ya
uongo na kutakatisha Dola za Kimarekani, 540,390 (sawa na Sh. Bilioni 1.181)
kutoka Kampuni ya Trade TJL DTYL Limited kwa madai kuwa angesambaza na
kusafirisha nje ya nchi kilo 207 za vipande vya dhahabu vyenye thamani ya Dola
za Kimarekani 8,280,000 lakini hakufanya hivyo.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitakatisha fedha
hizo zilizopatikana kwa njia ya jinai kwa kuelekeza kiasi hicho cha fedha
kuingizwa katika akaunti iliyopo benki ya Stanbic yenye jina la Kampuni ya Muru
Platnum na baadaye alizitoa zote na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi huku
akijua zimepatikana kwa njia ya udanganyifu.Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi
wa kesi hiyo bado haujakamilika na uliomba mahakama tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Nongwa alisema kesi hiyo itatajwa
Desemba 13, mwaka huu.Mshtakiwa alirudhishwa mahabusu kwa sababu mashtaka ya
kutakatisha fedha hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment