Snura anasema kipindi ambacho wimbo wake Chura unafungiwa kilikuwa cha misukosuko lakini aligoma kukata tamaa.
Akizungumza na mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove, Snura alisema neno kukataa tamaa halipo kwenye orodha ya msamiati wake.
“Kwenye
suala la kukataa tamaa kwangu halipo,” alisema. “Na kama ningekuwa ni
mtu wa kukataa tamaa ningekata tamaa kwenye Chura, lakini sikukataa
tamaa hadi kuhakikisha nairudisha na masekeseke ya chura yale
yaliyotokea yangenikatisha tamaa. Nimekutana na mambo mengi sana
kuhusiana na chura,” alisema.
Snura
anasema hasara iliyopatikana kutokana na kufungiwa kwa chura ilikuwa
kubwa kwakuwa ilikuwa na dalili za kuwaingizia fedha nyingi kwenye
Youtube ukiachilia deals zingine za show.
0 comments:
Post a Comment