-
Freeman Haikaeli Mbowe au kama tunavyomuita mtaani "MCHAGGA" ni rafiki
yangu wa karibu sana sana nimemfahamu toka utotoni na ndio maana mpaka
leo ninamuheshimu sana kwani ni mmmoja wa Binadam wachache sana
ninaowafahamu Duniani wenye msiamo na walio radhi kupoteza anything kwa
ajili ya msimamo. Toka utotoni Freeman hakuwahi kuwa mpenzi au shabiki
wa TANU au CCM, na sitashangaa kwamba hakuwahi kuwa hata Mwanachama ni
msimamo mzito aliokuwa nao kwamba TANU/CCM zilikuwa zinakosea na
zinahitaji kurekebishwa. Na ndio maana wakati ulipofika hakuwa na tatizo
kujiunga na Upinzani, yaani Chadema chama ambacho kilianza kwa kasi
sana chini ya Mzee Mtei, lakini kikashuka sana chini ya Marehemu Mzee
Makani na kikaja kuamka tena chini ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa sasa.
Amekichukua chama hicho kikiwa mahututi sana akapigana mpaka kukipa meno
na kuitingisha sana CCM, na cha msingi sana akafanikiwa kuwaingiza
Chadema Vijana wengi wenye misimamo kama yake ya Kipinzani na kukifanya
kuwa Chama kweli cha Upinzani na pia ni yeye ambaye amekifikisha chama
hicho kilipo sasa hoi bin taabani.
-
Freeman alikipatia uhai chama hicho kwa kujikita kwenye mbinu mbali
mbali za michezo ya kisiasa ambayo inakubalika kwenye lengo la
kuhakikisha ushindi na the end justifying the means, kwa mfano alikikuta
Chadema kikiwa na Wabunge wachache sana kulinganisha na sasa na the
number one mark ya Uongozi wa Freeman ambayo kama historia ya siasa na
Taifa hili itamkumbuka kwenye uongozi ni the FACT ya uongozi wake wa
Chadema kuweza kuwa attract Mawaziri Wakuu wawili wa zamani wa CCM,
kuwaunganisha Wapinzani karibu wote nchini under UKAWA katika kuikosesha
usingizi Serikali ya CCM..... lakini kwenye maisha kila chenye mwanzo
ni lazima kiwe na mwisho na hatimaye mwisho wa uwezo na akili nyingi za
Freeman kuongoza Upinzani wa kweli sasa zimeaanza kufika mwisho, Chadema
inahitaji Kiongozi mpya mwenye mbinu mpya kuweza kupambana na CCM.
-
Pamoja na makubwa yote aliyokifanyia Chadema kuna maamuzi mengi Freeman
aliyafanya kwa kucheza bahati nasibu ya Siasa ambayo matokeo hayakuwa
kama alivyotegemea lakini kuna faida kiasi fulani Chadema waliipata
kutokana na his gambling na hasa kwenye kuwapokea Mawaziri Wakuu 2 wa
zamani wa CCM, kwa upande mmoja alikiongezea Chama chake nguvu ya Muda
na pia kwa upande mwingine alikipunguzia chama chake nguvu ya muda
mrefu, isipokuwa cha msingi sana ni kwamba akiwa kwenye kilele cha
Utawala wake Freeman aliwekeza sana kwenye Media na Social Media ndio
the best political investment inayokibeba chama hicho sasa hivi wakati
kikiwa almost mwisho wa uhai wake. Kuwekeza kwake kwa Vijana wenye
msimamo na Media ndio kunakisaidia sana chama hicho kuendelea kupumua
mpaka leo huku the Natural Fate ikiwa inakipa nafasi chama hicho nafasi
ya kujikarabati ingawa Viongozi na Wanachama wengine wa Chama hicho
wanashindwa kuielewa hiyo concept.
-
Huu ni wakati muafaka wa Freeman kujiuliza kama je kuna nini ambacho
bado hajakifanya katika uwezo wake wa kufikiri na kuongoza Upinzani, kwa
sasa Chama hicho sio siri kimejipiga dhoruba kwa kamali ya kisiasa
aliyoamua kuicheza yeye mwenyewe Freeman kwa niaba ya Chama chake na
ndio maana ya Uongozi wa Taifa ni kwa Kiongozi kuwa na uwezo wa kuona
mbali kwa niaba anaowaongoza. Chadema imefika mahali inahitaji ukarabati
mkubwa sana na wa hali ya juu sana kuweza kurudi tena au kufikia zaidi
ya kilipokuwa huko nyuma. Chadema haina agenda yoyote tena zaidi ya
kusubiri Viongozi wa CCM wakosee herufi na maneno na kuanza kuyarudia
rudia kama utani badala ya hoja nzito kwa Umma ambao ulifikia hatua ya
kuwaamini sana nyakati fulani zilizopita. toka Utawala mpya wa Awamu ya
Tano ya CCM ushike madaraka Chadema imepwaya mno ni kawaida kwenye siasa
za Kitaifa ni kama chama cha Democrats huko USA na wao sasa hivi
wanakabiliwa na wakati kama huu wa Chadema ni wakati unaohitaji Viongozi
wake wa juu kujitafakari upya kama kweli wapo sawa na wanachohitajika
kukifanya yaani Upinzani.
-
Kutumia muda mwingi kuwashambulia kwa maneno ya mafumbo mafumbo na
lugha zisizokuwa za kistaarabu siamini kama inaweza kuisaidia Chadema
kurudi kwenye mstari wake wa kuaminiwa na Wananchi kama ilivyokuwa huko
siku za nyuma. Binafsi ninakubaliana sana na maneno ya Mwenyekiti Mao
Tse tung kuwa...... "Ukiona binadam wawili wanakubaliana kwa kila kitu
na kwa wakati wote ujue kwamba aidha Mmojawapo ni Mgonjwa au wote wawili
sio wazima".....Historia ya Dunia inaonyesha Chama kimoja kikikaa
madarakani kwa zaidi ya Miaka 50 huwa kunakuwa na tabia za kujisahau kwa
chama hicho so kinahitaji kukumbushwa kumbushwa kurudi kwenye mstari so
ni muhimu sana kuwepo kwa Upinzani nchini, lakini sio kwa huu upinzani
uliopo sasa. Freeman amekisaidia sana Chadema sana, lakini Chadema
ilipofikia sasa hivi nina wasi wasi ndio mwisho wa uwezo wake kufikiri
kisiasa ni wakati muafaka akatafakari kama ni wakati wa kufanya maamuzi
magumu sasa au kuja kujutia baadaye.
- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!
Le Mutuz Nation
|

0 comments:
Post a Comment