Bahati Bukuku amesema taarifa za kifo chake ni mbingu tu ndiyo
zitajua, kwa kuwa shetani hana nafasi ya kujua taarifa za kifo chake.
“Ni watu ambao wanaamini wakiongea hivyo watanipunguzia mashabiki,
mpango aliouandaa shetani hauwezi fanikiwa, kwa sababu kifo changu
shetani hatatangulia kujua ila Mbingu zitajua, shetani hana sababu za
kujua taarifa zangu”, Bahati Bukuku alikiambia kipindi cha Planet Bongo
cha EA Radio.
Bahati amesema tayari ameripoti kwenye vyombo husika vya uchunguzi ili kumchukulia hatua za kisheria mtu alianzisha uzushi.
0 comments:
Post a Comment