Hukumu hiyo ilitolewa Disemba 9 mwaka huu na hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama hiyo, Emmanuel Ngaile baada ya kuridhishwa na ushahidi wa
upande wa mashtaka. Waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo jela ni pamoja
na Augen Nicodem (41) mkazi wa Mkoa wa Kigoma, Mwita Marwa (27) na Amos
Alexender (25) wote wakazi wa wilaya ya Serengeti.
Hata hivyo adhabu hiyo imetokana na makosa sita ambayo yalikuwa
yakiwakabili ikiwemo kusafirisha silaha kinyume cha sheria, kumiliki
silaha bila kibali maalum, kuingia kwenye hifadhi bila kibali maalum,
kuuwa temba na mengine mawili.
0 comments:
Post a Comment