Mariah Carey amewaacha midomo wazi mashabiki zake kwa kusema kwamba hawafahamu wasanii hawa ambao wanamajina makubwa duniani.
Moja ya wasanii ambao walikuwa wakifanya vizuri sana na bado wanaendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki, namzungumzia Mariah Carey amewaacha hoi mashabiki zake baada ya kusema kwamba hawafahamu Ariana Grande, Miley Cyrus pamoja na Demi lovato.
Kupitia kipindi cha “Watch What Happens Live” kinachorushwa na Bravo, Mariah alisema kwamba kama mtu ajawahi kukaa nae na kuongea pamoja basi hawezi kumfahamu na ndio maana hawajui wasanii hao licha ya kuwa na majina makubwa katika Industry ya muziki.
“I don’t know her either so I wouldn’t say anything to her, She should come up, introduce herself to me, say, ‘Here’s my opinion. What do you think about it?’ That’s how you handle shit. Okay?”

0 comments:
Post a Comment