Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa Kenya Nchi Mhe. Ali Makwere, Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa Brazil Nchi Mhe. Carlos Alfonso Puente, Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa Denmark Nchi Mhe. E. Hebogand Jensen, Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia
Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Mhe. Maniza Zaman, mara baada ya
kumaliza mazungumzo,Ikulu jijini Dar es Salaam.
.................................................................
Mabalozi
wa Nchi Mbili za Brazil na Kenya wameipongeza serikali ya awamu ya Tano
kwa mipango na mikakati yake ya madhubuti ya kulifufua Shirika la Ndege
Tanzania -ATCL – kwa kununua ndege mpya kama hatua ya kuhakikisha
shirika hilo linakuwa bora katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga
ndani na nje ya nchini.
Mabalozi
hao wamesema hatua hiyo ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania
itasaidia kukuza shughuli za utalii na pato la taifa kwa ujumla.
Balozi
wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente na Balozi wa Kenya hapa nchini
Chirau Ali Makwere wametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na
kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es salaama.
Kwa
upande wake, Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente amesema
kutokana na nchi hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi kadhaa Dunia zenye
viwanda wa kutengeneza ndege hivyo serikali ya Tanzania ina nafasi nzuri
ya kununua ndege nchini Brazil hasa kulingana na mahusiano mazuri na ya
muda mrefu yaliyopo kati ya nchi hizo mbili.
Kufutia
wito huo wa Balozi wa Brazil Nchini, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametumia fursa hiyo
kuwakaribisha wawekezaji wa nchi ya Brazil kuja nchini kutangaza bidhaa
wanazotengeneza hasa ndege kama hatua ya kuimarisha mahusiano ya
biashara kati ya Brazil na Tanzania.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kutokana na nchi ya Brazil
kupiga hatua kubwa katika uzalishaji wa sukari na Tanzania ni moja ya
nchi yenye maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji huo hivyo ni muhimu kwa
wafanyabiasha wa Brazil kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta
hiyo.
Kuhusu
kilimo cha Pamba nchini, Balozi wa Brazil Carlos Alfonso Puente amesema
serikali ya nchi hiyo imeanzisha mradi kabambe unaolenga kusaidia
uzalishaji bora wa pamba katika mikoa ya kanda ya ziwa mradi ambao
utagharimu dola za Kimarekani milioni Sita kwa miaka minne nchini.
Katika hatua nyingine,
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mazungumzo yake na Balozi wa
Kenya hapa nchini Chirau Ali Makwere amesisitiza kudumishwa na
kuendelezwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya hasa
katika uimarishaji wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo Mbili.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito maalum kwa Watanzania
kuchangamkia fursa ya kufanya biashara na nchi ya Kenya kutokana na nchi
mbili kuwa na mahusiano mazuri ya kibiashara.
Wakati huo huo,
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Denmark nchini Hebogand Jensen ambaye amemweleza Makamu wa
Rais nia ya nchi hiyo kwa ushirikiano na nchi nyingine ya kujenga
kiwanda kikubwa cha mbolea wilayani Kilwa.
Balozi
huyo wa Denmark nchini amesema anaimani kiwanda hicho kitakachojengwa
nchini kitafanya uzalishaji mkubwa na kutoa ajira kwa mamia ya wananchi
wa Tanzania.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali katika
kuelekea kwenye uchumi wa viwanda imeweka mazingira mazuri kwa ajili ya
wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini kama
hatua ya kukuza uchumi wa nchi.



0 comments:
Post a Comment