"Kwa Saa 48 nimetafakari imani kubwa
aliyoionyesha kwangu mhe Rais John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Miongoni mwa mabalozi wetu,nimetafuta maneno muafaka ya kumshukuru na kumuonyesha ninavyoithamini imani yake kwangu lakini nimeyakosa.
Mhe Rais naomba upokee neno langu moja tu "ASANTE"
Nitafanya kazi kwa juhudi na maarifa kufikia matarajio yako kwangu. Kwa watanzania wenzangu nimepata maelfu ya salaam za kunipongeza na kuniombea kheri nawashukuru Sana, sitawaangusha. Mwisho Namshukuru Kipekee Mwenyezi Mungu kwa kufanya niendelee kuaminiwa naomba aendelee kunisaidia niilinde imani niliyoonyeshwa."


0 comments:
Post a Comment