Thursday, December 15, 2016

Tiptop Connection ni moja kati ya lebo za muziki ambazo ziliwahi kufanya poa sana kwenye game ya music hapa kibongo bongo, lakini ni ukweli usiofichika kwamba lebo hiyo kwasasa imedrop kiufanyaji kazi kulingana na ilivyokuwa zamani.

Ni maswali kemkem ambayo yalikuwa yakipelekwa kwenye uongozi wa lebo hiyo kutoka kwa mashabiki kuhusiana na ujio wa kazi zao mpya na vitu kama hivyo, lakini kwa sasa tumepenyezewa taarifa kuhusu maswali hayo kupungua kwa kiasi kikubwa sana.
Ni exclusive kutoka kwa Madee kiongozi wa lebo hiyo ambaye anadai kuwa brands za mavazi za lebo hiyo zimepunguza kwa kiasi kikubwa sana maswali kutoka kwa mashabiki kuhusiana na kazi mpya kutoka katika lebo hiyo.
“Kipindi cha kati watu walikuwa wanapiga makelele kuhusu Tiptop haipo, Tiptop hamna kitu ambacho kinasikika, zaidi watu wakawa wanataka nyimbo mpya za Tiptop, lakini zilivyotoka zile Poolover, T-Shirts, Kofia wamezigombania mpaka wamesahau maswali ambayo walikuwa wanatuuliza.”

0 comments:

Post a Comment