Kitaani kumekuwa na tetesi zinazo wahusisha producer wa The Industry Nahreel na kundi la Weusi kuwa hawapo katika maelewano mazuri.
Tetesi ambazo zimeanza kuchukua nafasi baada ya kuona kundi la Weusi kuwa linafanya kazi nje ya studio za The Industry tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Tetesi hizo zilipelekea hadi kuzuka uvumi kwamba producer Nahreel ndiye ambaye ameuzuia wimbo wa Joh Makini ambao kamshirikisha Davido, kutokana na wimbo huo kuzungumziwa kwa muda mrefu lakini mpaka sasa haujaweza kuachiwa.
Sasa producer Nahreel amebonga na kipaza cha E-News ya EATV na kufunguka kila kitu kuhusiana na tetesi hizo.
“Sisi hatujazuia, kwanini tuzuie ngoma ya Joh Makini na Davido? Hii ngoma inaenda kutoka na Joh makini amekwisha shoot video, kwahiyo stay tune, inaenda kutoka.” Alisema Nahreel.
Nahreel pia aliongeza kuwa zipo ngoma kibao za Joh Makini ambazo zipo kwenye studio yake, ikiwemo na ngoma ambayo Joh Makini amefanya na Khuli Chana wa South Africa.
“Zipo ngoma kibao, Joh Makini ana ngoma na Khuli Chana ipo pale, pia kuna nyingine ambayo sitaki kuitaja ipo pale, pia G Nako na Nikki wa Pili nina ngoma zao kibao. Nadhani huu mwaka nili focus sana na mambo ya The Industry kama Navy Kenzo na wasanii wake ndio maana kidogo watu waliona kuna umbali, lakini kibiashara tuko vizuri, tuko fresh kabisa na ngoma zinaendelea kama kawaida.” Aliongeza Nahreel.
Nahreel pia alikanusha kabisa uvumi uliodai kuwa Weusi wanafanya kazi kwake for free na kudai kuwa Weusi wamekuwa wakimlipa kwa muda wote.

0 comments:
Post a Comment