Mkali kutoka WCB Wasafi Richard Martin almaarufu kama Rich Mavoko amefunguka hisia na mapenzi yake juu ya ngoma nyiingine za Bongo Fleva jinsi anavyo zikubali na ambavyo huwa anazipokea pia.
Mkali huyo ameiambia alizungumza na XXL kuwa kama angekuwa na uwezo wa kufanya remix basi ngoma ya Kamatia Chini ya kwao Navy Kenzo ingemuhusu, kwasababu ni ngoma ambayo anaikubali na pia anaisikiliza mara kwa mara kiasi kwamba amekwisha kuitungia verse.
“Navy Kenzo wangesema kama kuna remix ya Kamatia Chini inatoka, ningeua, kwasababu nina verse tayari na endapo tu wakisema kama kuna remix basi itakuwa ni ngoma kubwa sana.” Alisema Rich Mavoko
Unajua vile midadi haiwezi kusimulika eeh? Sasa nimekuletea hii video hapa chini ili uweze kuplay uisikie midadi ya Rich Mavoko wakati akijitapa kuwa na verse ya Kamatia Chini.

0 comments:
Post a Comment