Msanii wa Bongo Fleva dully sykes ameweka wazi mipango yake ya kulifikia soko la international
Akipiga story na Planet bongo ya EA Radio Dully amesema kwamba hata hapa kuna wasanii wa International hivyo mipango yake ni kufanya nao kazi ili iwe rahisi kwake yeye kuvuka mipaka na kutambulika kiurahisi
"Hata hapa tuna International, tuna wasanii ambao washafika international, lakini ningefikiria kwanza niwaanzie wa hapa ili hawa wa hapa wanitangaze kule ili iwe rahisi mimi kwenda
nao kule, umeshanielewa sijui point yangu?" alihoji Dully sykes "inabidi niwashirikishe wa hapa ili wa hapa wanifikishe kule halafu wale wa kule iwe rahisi kama mimi sijawaomba kufanya nao kazi basi wao wataniomba mimi"
Mkali huyo wa inde amefunguka kuhusu ngoma yake na Diamond platnumz imefikia wapi na hatua aliyofikia kuhusu kufanya kazi na hao wasanii wa hapa ambao washafika international
"Mimi na Diamond huwa hakuna shida yani ni kama nyanya na kitunguu kwenye mchuzi lazima vitakuwepo tu kwahiyo sijaamua kusema ni utoe, kwa sababu kabla ya Inde ilitakiwa
tutoe wimbo wetu mimi na Diamond kwahiyo sijaamua alisema Dully "nina nyimbo nyingi nzuri ikiwemo huo wimbo wangu na Diamond, pia nina nyimbo mimi hapa Ray vanny na Rich mavoko kwahiyo nitajua nitafanya vip, pia nina wimbo na Vanessa mdee
kwahiyo nitajua upi utoke upi uanze kwasababu zote ni nyimbo nzuri"
Dully amemaliza kwa kusema kwamba bado anatengeneza mazingira ya hapa nchini kwake kwaajili ya kulifikia soko la nje
0 comments:
Post a Comment