Monday, January 16, 2017

Ikiwa ni baada ya siku chache Young killer kuachia ngoma yake ya sinaga swaga ambayo imezua utata kwa baadhi ya mistari ya ngoma hiyo ikiwemo ule usemao "wanasema joh anabebwa mpaka nahisi ni ukweli"


Msanii mkongwe wa bongo fleva ambae kwa sasa anatamba na kibao chake yono amefunguka mtazamo wake juu ya ishu ya young killer kumdiss Joh makini .

"Kwa upande wa joh makini yule atakuwa kamvunjia heshima kwasababu joh makini ni kaka yake lakini pia tukirudi kwenye upande mwingine unajua young killer ni msanii ambae alikua ndio anakuja anafanya vizuri ila  hapa katikati kama alidrop nafikiri hii ni njia nzuri pia kwake yeye kumrudisha kwenye nafasi" alisema Dully sykes kwenye planet bongo ya East Afrika Radio

0 comments:

Post a Comment