Tuesday, January 17, 2017

Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
Matarajio ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya kumtumia mwanaye Nillan kupata mamilioni ya pesa kutoka kwa wadhamini yanadaiwa kubuma kufuatia maelezo kuwa, baadhi ya makampuni yaliyokuwa yamezungumza naye yameamua kujiweka pembeni kutokana na ukata wa pesa.Awali, akizungumza hivi karibuni, Diamond aliweka wazi kuwa, kabla hata mtoto hajazaliwa kuna benki mbili ambazo zilimwaga dau la mamilioni ya pesa kwa ajili ya kutumia picha ya mtoto huyo kwenye huduma zao lakini yeye alikuwa hajaweka wazi ipi aingie nayo mkataba na kwa mkwanja upi.

0 comments:

Post a Comment