Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameipongeza halmashauri YA chunya kwa kuwa YA kwanza kimkoa kwa ukusanyaji mapato na kutoa mikopo kwa Vijana na wanawake
Hayo ameyasema Leo wakati wa kikao cha kujadili TAARIFA YA mkaguzi Mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali wilayani Chunya

Pamoja na pongezi hizo ameutaka uongozi wa halmashauri YA Chunya kugawa na kutangaza hadharani vikundi vitakavyopata mikopo hiyo

Amesema kutoa mikopo hiyo kimyakimya inazusha minongono hivyo ni vema mikopo hiyo itoke we hadharani ili wananchi wajue jitihada zinazofanywa na serikali yao

Amewataka maafisa wahusika kutoa Elimu kwa vikundi na zaidi wananchi kuelewa kuwa mikopo hiyo siyo bure inarejeshwa ili na wengine waweze kupata



0 comments:
Post a Comment