Tuesday, January 3, 2017


Wema Sepetu hayupo peke yake linapokuja swala la kufuta posti zote katika kurasa ya Instagram mwaka mpya ulivyoanza, rapper Future ameungana na mrembo wetu kwenye listi ya kufuta posti zote kwenye Instagram.

Baada ya kuachia ngoma yake na Rick Ross ya “That’s A Check” siku chache zilizopita, nyota huyo wa Atlanta namzungumzia Future ameamua kuisafisha Instagram page yake kwa kufuta kila kitu na kuuanza mwaka 2017 akiwa msafi kwenye Instagram page yake, jambo hili limewafanya mashabiki kuamini kwamba kuna ujio mpya wa ngoma kibao kutoka kwa Future, ndio mana imepelekea kufanya hivi.
Tukirudi nyumbani Bongo pia tunakutana na Sweetheart mwanadada Wema Sepetu, ambaye naye aliamua auanze mwaka mpya akiwa na posti za mwaka huu, sasa ili kufanya hivyo, Instagram page yake ikabidi isafishwe na yeye kwa kufuta posti zote, hakuna anayejua kwanini Wema Sepetu amefanya ishu hiyo ya kufuta posti zake zote.


0 comments:

Post a Comment