Wednesday, January 18, 2017

Kama unafatilia akaunti ya belle 9 na pia unafatilia akaunti ya Ridhiwani Kikwete picha za Belle 9 kwenye akaunti ya Ridhiwani utakua umeziona na picha za Ridhiwani kwenye akaunti ya belle pia utakua umeziona,inawezekana ukaanza kujiuliza kama wameanza kufanya kazi pamoja au ni picha tu.


Ridhiwani kakubali kufunguka kuhusu picha hizo na kama kuna makubaliano yoyote ya kumsimamia Belle 9 >>’Hapana mimi sim-manage Belle 9 ila wiki nne zilizopita kama siyo tano nilikua naangalia kwenye Instagram page yangu mmoja wapo katika ya watu ninao-wafollow ni Belle 9 alikuwa amepost picha ambayo anaonyesha yuko South Africa akiwa anafanya recording,Mimi kwangu nilipomuona anarecord muziki wake nikavutiwa sana,siku aliporudi hapa Dar es salaam nikamtafuta ili niweze kukutana naye,nilikutana naye kama ninavyokutana na vijana wengine kujaribu kujua mziki wake unakwendaje lakini pia na sisi kama vijana tuliopata nafasi ya kuwa viongozi tunaweza vp kuwasaidia,baada ya mazungumzo kilichotokea akawa amependa zaidi mazingira ya hapa kwangu akasema bwana brother kama hutojali ningeomba nafasi ya kufanya launching au listening party ya wimbo wangu wa “Give to me” nikamwambia mzee mimi sina tatizo karibu sana hapa ni kwako’.

0 comments:

Post a Comment