Lebo ya WCB Wasafi inazidi kukua kila kukicha kwani mbali na kusaini wasanii lakini pia tumeona wakijitahidi kupiga hatua mbalimbali kama kudhibiti mapato kwenye mitandao ya kijamii kama youtube haya yote ni mafanikio.
Good News ni kwamba Lebo hiyo maarufu nchini imeshakamilisha kandarasi ya ujenzi wa Ghorofa ambalo litaitwa ‘WCB TOWER’,Wakithibitisha ujenzi huo kupitia mtandao wa Instagram Mameneja wawili wa Diamond Platnumz ambae ndiye muanzilishi wa Lebo hiyo wamesema Kila kitu kipo tayari na wameshakabidhi kwa mkandarasi kinachosubiriwa ni ujenzi tu uanze.
“Ujenzi wa WCB Tower karibia kila kitu kipo tayari kinachosubiriwa ni mkandarasi kuanza kazi“Alijibu Sallam swali aliloulizwa na Mdau mmoja kwenye mtandao wa Instagram.
Hata hivyo bado haijajulikana ni lini ujenzi huo utaanza na ni eneo gani hapa jijini Dar es salaam jengo hilo refu litajengwa?Baki na sisi tukujuze vitu vyote vinavyoendelea kuhusiana na ujenzi huo pamoja na habari kemkem za Burudani.

0 comments:
Post a Comment