Wednesday, January 18, 2017


Kama unakumbuka tarehe 09 November 2016 ilitoka taarifa rasmi kutoka MTV Ema kuomba radhi kwa kuchanganya tuzo aliyotakiwa kupewa Alikiba lakini kwa bahati mbaya akapewa Wizkid,Ni muda mrefu umepita mpaka sasa ikiwa tuzo hiyo bado haijamfikia Alikiba.


Kupitia XXL ya Clouds FM mmoja kati ya viongozi wa Alikiba ametolea ufafanuzi suala hilo>>‘Nafikiri hata mkiangalia kwa washindi wa nyuma ambao waliwahi kushinda kutoka Tanzania inachukuaga muda kumfikia mshindi,ni process ambazo wenyewe Mtv Ema wamejipangia,Nachofikiri ni process zao tu lakini tunawasiliana nao wametuambia watatutaarifu lini itafika either tukaipokee South Africa au watutumie,unajua kipindi tuzo tunashinda kulikuwa na hollyday si unajua wazungu walivyo ikifikia karibu na mwishoni mwa mwaka huwa wanakwenda hollyday ofisi nzima zinafungwa,Sasa hivi mwaka umeanza watu office wamefungua tutapata jibu soon na tutawajulisha,tuzo iko fresh itakapofika kila mtu ataiona’

0 comments:

Post a Comment