Sunday, January 1, 2017

Mkali wa bongo fleva kutoka WCB Wasafi Harmonize, amefunguka kuhusu mahusiano yake na staa wa bongo movie, Jackline Wolper na kusema kuwa mahusiano hayo hayajamrudisha nyumba kimuziki kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Harmonize amefunguka hayo akiwa kwenye kipindi cha FNL ambapo amesema kuwa kazi zake ziko palepale na hakuna kilichoharibika kwa kuwa amekuwa kwenye muziki kabla ya mahusiano hayo ambayo yameanza mwaka huu.
Pia amesema mahusiano aliyonayo na Wolper na 'real' na wala hayana lengo la kutafutia 'kiki' huku akikanusha kuhusu tetesi za Wolper kuwa na ujauzito pamoja na tetesi za yeye kuwa demu mwingine wa kizungu
"Jacky hana mimba, na mimi sina demu wa kizungu, sina mwanamke mwingine tofauti na Jacky maana huwezi kuwa na wake wawili"
Jackline Wolper
Akiuzungumzia mwaka 2016, Harmonize amesema hatausahau kwa kuwa umekuwa ni a mafanikio makubwa kwake ikiwemo kupata tuzo tatu nje ya Tanzania ikiwemo ya 'Best New Comer Africa' aliyoipata wiki hii.
Mkali huyo wa ngoma za Bado, na matatizo leo hii amealikwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwenda kusherehekea pamoja siku kuu ya Mwaka Mpya, nyumbani kwake Msoga, Bagamoyo

0 comments:

Post a Comment