Wednesday, January 4, 2017

Mkali wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim ‘Wizkid’, amedai anatarajia kufanya makubwa 2017 na hana mpango wa kuangalia aliyoyafanya 2016.

WizKid
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26, alifanya makubwa mwaka 2016, kwa kufanya kazi na nyota wakubwa wa muziki duniani akiwemo, Drake na Chris Brown.
“Mwaka jana nilifanya makubwa pamoja na kununua nyumba nchini Marekani, lakini mafanikio hayo si kitu chochote kwangu, natarajia kufanya makubwa zaidi kwa mwaka huu”.
“Kwa sasa nipo katika mapumziko hadi Februari mwaka huu, sina mpango wa kuangalia nilipotoka, nataka niwe kama nimezaliwa upya huku nikiwa na kiu ya mafanikio,” aliandika Wizkid.
Mbali na hilo, Wizkid ni miongoni mwa wasanii waliotajwa kuwania tuzo ya Grammy 2017 kupitia kushiriki kwenye album ya Drake, Views.
Wizkid alishirikishwa kwenye wimbo One Dance uliomo kwenye album hiyo iliyotajwa kuwania kipengele cha Album ya Mwaka. Inachuana na album za Adele, Beyonce, na Justin Bieber.

Hawa ndio waliotajwa pamoja kwenye album ya Views kwa mujibu wa Grammy:

Drake – Views
dvsn, Future, Kyla, PartyNextDoor, Rihanna & Wizkid, featured artists; Brian Alexander-Morgan, Axlfoliethc, Beat Bully, Boi-1Da, Cardo, Dwayne “Supa Dups” Chin-Quee, Daxz, DJ Dahi, Frank Dukes, Maneesh, Murda Beatz, Nineteen85, Ricci Riera, Allen Ritter, Noah “40” Shebib, Southside, Sevn Thomas, Jordan Ullman, Kanye West, Wizkid & Young Exclusive, producers; Noel Cadastre, Noel “Gadget” Campbell, Seth Firkins, David “Prep” Bijan Huges & Noah “40” Shebib, engineers/mixers; Chris Athens, mastering engineer
Label: Young Money/Cash Money/Republic Records

0 comments:

Post a Comment