Thursday, February 23, 2017

Issa Hayatou - Rais CAF

Rais wa Shirikisho la soka barani Africa CAF Issa Hayatou amemueleza rais wa FFA Gian Infantino kwamba bara la Afrika linahitaji kupatiwa nafasi 10 za ushiriki katika fainali za kombe la dunia kuanzia mwaka 2026.

 
Ombi hilo limekuja kutokana na mpango uliopo wa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki katika fainali za kombe la dunia kutoka 32 na kufika 48.
 
Mchakato wa kuongezwa kwa timu hizo umeanza katika mkutano wa siku tatu baina ya Rais wa FIFA Gian Infantino na zaidi ya viongozi 50 toka katika vyama mbalimbali na mashirikisho ya soka barani Afrika.
 
Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa aina hii kufanyika barani Afrika.
Gian Infantino - Rais FIFA

 
Kwa sasa Bara la Afrika lina nafasi tano tu katika kombe la dunia na idadi ya timu hizo ndio zitakazoshiriki katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 nchini Urusi pamoja na mwaka 2022 huko Qatar.
 
Wakati bara la Afrika likianza mchakato wa kuhakikisha linapata nafasi 10, Barani Ulaya upo mchakato wa kutaka kupewa nafasi ya timu kuingiza kati ya timu 13 hadi 16 katika kombe la dunia.
 
Asia wanataraji kuomba kuingiza timu nane.

0 comments:

Post a Comment