Tuesday, February 7, 2017

Wakati sakata la madawa ya kulevya linaendelea kuunguruma kila kona ya nchi na kuwajumuisha wasanii maarufu nchini, haswa wa Muziki na filamu, ‘Esmaplatnumz’ ambaye ni dada wa mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amefunguka juu yawanaoshikiliwa na polisi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esma kapost ujumbe wa kuwapa pole watu wa karibu na familia yake wakiwemo marafiki wanaoshikiliwa na polisi kuhusiana na suala hilo.
Esma
“Ndugu zetu wa karibu na familia yetu, tunawapenda sana, inshallah Allah atafanya wepesi kwenye jambo hili” ulisema ujumbe huo.
Esma ambaye anafahamika kama mke wa ndoa wa meneja maarufu wa wasanii, Petit ‘Petiman Wakuache’, ambaye wanamtoto mmoja wa kike aitwaye Taraj.

0 comments:

Post a Comment