Leo kwenye kipindi cha Leo tena cha Clouds FM Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari walikuwa na xclusive interciew kwenye kipindi hicho ikiwa ni kuelekea 40 ya mtoto wao wapili ambaye amepewa jina la Nillan.
Ni mengi ambayo wameyaongelea wawili hao lakini kubwa zaidi ni kuhusiana na shughuli hiyo ya 40 ambayo inatarajiwa kufanyika jumamosi hii nyumbani kwa Diamond platnumz Tegeta Dar es Salaam.
Wametusanua kwamba katika shughuli hiyo watakao ruhusiwa kupenya ni wale ambao wamealikwa tu, bila kujali nani wala nani kama haujaalikwa huwezi kupenya katika shughuli hiyo.
Kitu ambacho kimewashangaza kama sio kuwafurahisha wengi ni pale wawili hao walipo zungumza kwamba wamemualika Wema Sepetu kwenye shughuli hiyo.
Ikiwa inafahamika fika kwamba Wema Sepetu alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz na kuna kipindi hapa katikati tulikuwa tukishuhudia kutokuelewana kwa Zari na Wema Sepetu.
Play hii video hapa chini kumsikiliza Diamond Platnumz akifunguka juu ya mualiko huo wa Wema Sepetu.

0 comments:
Post a Comment