Thursday, February 9, 2017

Diamond Platnumz amezidi kuendelea kutengeneza rekodi kwenye muziki wake, na hii ni mpya kupitia ngoma yake aliyomshirikisha Ne-Yo kutoka Marekani, “Marry You”.

Rekodi hiyo mpya ni kutoka kwenye ‘Marry You’ kufikisha idadi ya views Milioni 1 ndani ya siku 5 toka iachiwe na hatimae Diamond Platnumz kuwa msanii wa pili Tanzania kwenye mtandao wa VEVO kuwa na video iliyotazamwa zaidi ya mara 100 nyuma ya Vanessa Mdee ambae nyimbo zake mbili zimefikisha views zaidi ya Milioni 1.1.
diamond
Ikumbukwe kuwa ngoma hiyo mpya ‘Marry You’ yakwake Diamond Platnumz ipo kwenye akaunti yake mpya ya VEVO na ndiyo ngoma yake ya kwanza kuitupia kwenye mtandao huo.

Vevo ni nini

vevo_logo_detail
VEVO ni mtandao wa internet unaoshughulika na video za muziki na wanamuziki unaomilikiwa na kampuni kubwa za muziki duniani SONY Music Group, Universal Music Group, Warner Music Group na Google. VEVO ni mtandao number moja duniani unahusika na kuhifadhi na kurusha kazi za muziki za wanamuziki maarafu duniani, kama Jay Z, D’banji, Nick Minaj, Mafikizolo na wengine wengi.

0 comments:

Post a Comment