Posted by Williammalecela.com on Wednesday, February 08, 2017
Rapa Kanye West auvunja rasmi urafiki wake na Rais wa Marekani Donald Trump. Umeripoti mtandao wa TMZ.
Kwa ushahidi uliobainika ni Kanye kufuta Tweets zote alizokuwa akimsifia na kuonesha imani na Rais huyo.
TMZ wameripoti kuwa chanzo ni Kanye kuchukizwa na vitendo vinavyo endela kwa Trump kukataza baadhi ya mataifa ya kiislamu kuingia nchini humo.
Mapema mwezi Disemba mwaka jana, rapa Kanye West aliingia kwenye headlines za dunia kwa kutangaza na kuonesha mapenzi yake kwa Trump, pale alipoipeleka miguu yake Trump Tower na kukutana na Rais huyo adui wa Wamarekani Weusi.
0 comments:
Post a Comment