Posted by Williammalecela.com on Wednesday, February 08, 2017
Headline za Bongo Fleva mwaka 2017 ni kila msanii kuapa kuanza kufanya album. Mmoja wa waliokula kiapo hicho ni Rais wa Manzese MADEE.
Akizungumza kwenye kipindi cha EIGHT cha TV-E, Madee amesema album hiyo itakuwa ya tofauti kwani atafanya ushirikiano na Dogo Janja,
"Katika kitu tulicho wadhulumu Watanzania ni kuwanyima album, mimi upande wangu mpaka sasa nina album 3." Alisema Madee
.
"Lakini mwezi wa 6 mwaka huu kuna album itatoka, inaitwa "MADO" yani Madee na Dogo Janja, itakuwa ni album ya pamoja na Dogo Janja."- alimaliza Madee ambaye anayasumbua masikio na macho yetu kwa Hit yake, HELA.
0 comments:
Post a Comment