Tuesday, February 28, 2017


Mcheza tennis namba 10 kwa ubora duniani Roger Federer amefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wa kwanza kwenye mashindano ya mabingwa ya Dubai kwa kumtandika Mfaransa Benoit Paire ndani ya dakika 54.


Katika mchezo huo Federer raia wa Uswi alipata ushindi wa seti 6-1 6-3 na sasa anamsubiri mshindi kati ya Mikhail Youzhny au Evgeny Donskoy.
Kwingineko mchezaji nambari moja kwa ubora duniani, Andy Murray pamoja na Nenad Zimonjic wamepoteza katika mchezo wa wachezaji wawili kwa wanaume mara baada ya kukubali kichapo cha seti 6-1 7-6 (7-2) dhidi ya Dan Evans na Gilles Muller katika mzunguko wa kwanza.
Mara baada ya kupoteza katika mchezo huo, Andy Murray sasa atashuka tena uwanjani kumkabili Malek Jaziri, kutoka Tunisia.

Hii ni mara ya sita kwa Murray kushiriki katika mashindano ya Dubai na hatua kubwa aliyowahi kufika katika mashindano hayo ni kufika katika fainali za mwaka 2012, hata hivyo alipoteza mbele ya Roger Federer.

0 comments:

Post a Comment