Mkurugenzi wa Mashule
watoto na walemavu katika mchezo wa mpira wa kikapu Charles Misoji amesema ligi
ya mchezo wa wa kikapu kwa jiji la Dar es Salaam imekuwa na ushindani mkubwa
tofauti na msimu uliopita.
Misoji amesema ushindani umekuwa mkubwa sana na ni vigumu
kufahamu ni timu ipi itakayopata ushindi katika michezo inayoendelea, kwani
timu shiriki zimeonekana kujipanga kuwania ubingwa.
Katika hatua nyingine
misoji amesema maandalizi kwaajili ya ligi daraja la pili yameshaanza huku timu
zaidi ya 24 zikitarajiwa kushiriki.
Misoji amesema kwamba
katika ligi hiyo viwanja vilivyopo pembezoni mwa mji ndio vitakavyotumika ili
kuutangaza zaidi mchezo wa mpira wa kikapu.

0 comments:
Post a Comment